Chama cha kiswahili maseno kushiriki tamasha na kongamano la kukata na shoka wiki lijalo katika chuo kikuu cha Laikipia ,kongamano la CHAWAKAMA Kenya.

Kongamano hill linanawiri kukikuza talanta na kiswahili nchini kenya na nchi mbalimbali barani Afrika,kauli mbiu likiwa tukienzi kiswahili ,kongamano hilo litaandaliwa mnamo tarehe 6 na 7 chuoni Laikipia .

Siku zote waswahili husema ukiona vyaelea jua vimeundwa na mbiu ya mgambo ikilia siku zote jua Kuna jambo .

Mwenyekiti CHAKIMA maseno amehimiza wanachama wote kuonyesha talanta zao mbalimbali kwa njia ya mashairi ,maigizo na kadhalika.

Vile vile Naibu mwenyekiti Moses okelo na pia mwandishi wa mashairi na vitabu mbalimbali asisitiza msimamo wa kuwa kiswahili siku zote kitukuzwe na pia kiswahili chalipa huku akitolea mfano mbalimbali katika nyanja ya uandishi.Hivyo wapenzi wote wa kiswahili waalikwa na hawana budi ila kuitikia wito huo,siku zote twasema dunia rangi rangile na kua maisha ni mshumaa ,hupangwa na Mtendawazi na kalamu yake siku zote haikosi.